Video Queen matata Bongo, Agnes Jerald ‘Masogange’.
VIDEO Queen matata Bongo, Agnes Jerald ‘Masogange’ amefungua mdomo
wake na kuwaka kuwa anachukizwa na tabia ya baadhi ya watu ambao
wanatumia jina lake kutapeli kwenye mtandao wa kijamii wa Facebook.
Akizungumza na mwanahabari wetu, Masogange alisema kuwa watu
wanaotumia jina lake wakome kwa sababu wanamjengea hisia tofauti kwa
watu wakati yeye hanufaiki na chochote.
“Kwa kweli inauma sana mtu kutumia jina langu kwenye mitandao halafu
halitumii kwa uzuri, kazi ni kuomba pesa kwa watu mbalimbali, jamani
mimi situmii mtandao wa Facebook kabisa kwa hiyo watu wawe makini,”
alisema Masogange.
Post a Comment