Nasibu Abdul ‘Diamond’akiwa kwenye pozi na mtoto mzuri kutoka Uganda, Zarina Hassan ‘Zari The Boss Lady’.
STAA anayetamba na ngoma mpya ya Nitampata Wapi, Nasibu Abdul ‘Diamond’
na mtoto mzuri kutoka Uganda, Zarina Hassan ‘Zari The Boss Lady’
wameoneshana malovee hadharani na kuwaacha watu midomo wazi.
Tukio hilo lililoacha historia ya aina yake kwa kutokana na umaarufu wa
wawili hao, lilitokea Jumatano iliyopita, nchini Uganda wakati Zari
alipokwenda kumpokea Diamond katika Uwanja wa Ndege wa Kampala nchini
humo.
‘Zari The Boss Lady ‘Diamond wakipata ukodaki.
Kwa mujibu wa chanzo kilichoambatana na Diamond, Zari alimpokea mgeni
wake kwa mabusu motomoto na msafara wa kwenda hotelini ulipoanza,
walipewa ulinzi mzito hadi hotelini ambako kila wakati wawili hao
walipeana mabusu ya kiaina kuonesha ‘wamemisiana’.
Alipotafutwa Diamond kwa njia ya simu ya mkononi, hakutaka kufungukia
mahaba hayo yaliyozua gumzo zaidi ya kucheka na kusema amejiandaa
vilivyo kumpa sapoti Zari katika shoo yake ya All White Part
iliyotarajiwa kufanyika juzi nchini humo.“Mwanangu nimejipanga, kitanuka
mbaya katika hii shoo si unajua huwa sirudi nyuma?” alisema Diamond.
Post a Comment