 SIKU
 chache kabla ya kupatwa na umauti, mnenguaji mkongwe Bongo, Mwanaisha 
Mbegu ‘Aisha Madinda’ alifunguka maneno ambayo yalionesha dhahiri kama 
alikiona kifo chake. Kwenye mazungumzo hayo aliyozungumza na mwanahabari
 wetu, Aisha alisema atatoa habari nzito ambazo zitaripotiwa na magazeti
 matatu na kudai ni ‘sapraiz’.

Mnenguaji
 mkongwe Bongo, Mwanaisha Mbegu ‘Aisha Madinda’. Licha ya paparazi wetu 
kumdodosa aseme habari hizo, alikataa na kusema itakuwa ni  
sapraiz.“Nina furaha sana kwa sababu nimerudi salama kutoka Dubai 
nilikokuwa nalazimishwa kufanya kazi za ndani nikakataa, ukweli watoto 
wangu wamefurahi sana kwa sababu nimerudi nikiwa na afya njema. 
“Niko fiti nimeachana na madawa ya kulevya sasa hivi nimerudi rasmi 
kwenye kazi yangu ya unenguaji, nitakutafuta siku nikupe habari kubwa 
ambayo sijawahi kuzungumza sehemu yoyote yaani itakuwa ni nzuri na 
utatoa magazeti matatu,” alisema Aisha ambapo Desemba 17, mwaka huu 
alifariki dunia kabla ya kutimiza ahadi hiyo kwa mwandishi wetu.Aisha 
aliyeacha watoto wawili wa kiume na wa kike, alitarajiwa kuzikwa jana 
nyumbani kwake Kigamboni, jijini Dar.
 
Post a Comment