Msichana 
wa kazi aliyetikisa vyombo vya habari duniani kwa kumtesa mtoto wa miezi
 18, Arnella Kamanz aliyekuwa kwenye uangalizi wake huko Uganda, amekiri
 makosa mbele ya mahaka nchini humo.
Jolly
 Tumuhiirwe, mwenye umri wa miaka 22, alifanya ukatili uliochukiwa na 
watu wote Duniani, ambapo alinaswa na camera ya siri, akimtandika mtoto 
wa mdosi wake kwa kumkanyaga mgongoni akiwa ameanguka chini, kumchapa na
 kitu kisichojulikana na kumpiga mateke na makofi ya nguvu usoni.
Kitendo 
hicho kilifuatia mtoto huyo wa kike, kushindwa kula, kutokana na kasi ya
 ulishwaji ambapo Tumuhiirwe, alikuwa akimlisha mtoto huyo kwa kasi ya 
ajabu, kwa kushindilia vijiko mdomoni mfululizo.
Huenda 
mahakama hiyo ikamuhukumu kifungo cha hadi miaka 15 jela, kulipa faini 
au vyote kwa pamoja. Msichana huyo katika maelezo yake mahakamani, 
aliomba radhi wazazi wa mtoto huyo, taifa la uganda na walimwengu wote 
waliokereka na kitendo chake na kuomba msamaha. Hukumu yake itatolewa 
Jumatano Desemba 11, 2014.
Hata 
hivyo wakili wa msichana huyo wa kazi aliyekiri kosa hilo Desemba 8, 
2014, amedai kuwa mteja wake hakutendewa haki kwa vile hakuelewa 
mashtaka yaliyokuwa yakimkabili.
Arnella Kamanzi, binti mrembo na mcheshi mwenye umri wa miezi 18 tu, aliyeteswa na Tumuhiirwe
 

Post a Comment