Stori: Imelda Mtema MSANII
 aliyefariki dunia hivi karibuni mjini Morogoro, Sherry Magali, anadaiwa
 kuwa alikuwa akilitaja jina la Ruth Suka ‘Mainda’ kila mara hadi 
alipofikwa na umauti.
Marehemu Sherry Magali enzi za uhai wake.
Chanzo chetu makini kilichokuwa karibu na 
msanii huyo wa filamu, kinasema Sherry alianza kugoma kula akidai hadi 
amuone msanii mwenzake huyo ambaye alikuwa jijini Dar es Salaam 
anakoishi.
Msanii wa 'Bongo Movie' Ruth Suka (Mainda) akiwa katika pozi.
Mpashaji huyo alisema hata siku aliyofariki
 pia alilitaja jina hilo, kitendo kilichowaumiza sana baadhi ya ndugu na
 marafiki. Mainda ambaye alikuwa ni rafiki wa marehemu, alikiri kusikia 
jambo hilo na anasikitika kwamba siku aliyopanga kwenda, ndiyo ambayo 
mwenzake alifariki.
 
Post a Comment