Kabla mwaka 2014 haujaisha idadi ya watu maarufu wa Tanzania
waliotangulia mbele za haki imezidi kuongezeka na hii ni baada ya
taarifa kutoka Iringa zilizoanza kusambaa kuanzia saa tatu usiku
November 11 2014.
Taarifa zilizothibitishwa ni kwamba rapper Geez Mabovu ambae ni
maarufu kwenye muziki wa hiphop Tanzania, amefariki dunia kwenye
hospitali aliyokua amelazwa nyumbani kwao Iringa alikokwenda wiki mbili
zilizopita kutokea Dar es salaam.
Hii
ni picha ya July 2013 ambayo ni mara ya mwisho Geez Mabovu ameonekana
kwenye millardayo.com akiwa na Baba yake Dully Sykes maeneo ya Kinondoni
Dar es salaam nje ya Bar ya msanii Dudubaya aliyokua ameifungua wakati
huo.
Post a Comment