NDOA ndoano! Staa wa sinema za Kibongo, Jacqueline Steven Pentzel ‘Jack Pentzel’ na mumewe Gardner Dibibi wanadaiwa kukinukisha na kuingia kwenye gogoro la kila siku hadi mwanaume kutaka kuondoka nyumbani wanakoishi Mbezi-Shamba jijini Dar.
Kikizungumza
na Ijumaa Wikienda, chanzo makini ambacho ni mtu wa karibu wa wanandoa
hao, kilisema kwamba, kila kukicha wawili hao wamekuwa wakigombana na
sababu kubwa ni Jack kuchelewa kurudi nyumbani.
Ilidaiwa
kwamba, tangu Jack awe na ushosti na staa mwenzake wa sinema za
Kibongo, Rose Ndauka amekuwa ni mtu wa kujiachia na kujisahau kwamba ni
mke wa mtu. “Yaani ndoa ya Jack inashikiliwa na uzi kwani kila siku
wanapigana na hivi karibuni mumewe alikusanya nguo na kuweka kwenye begi
akitaka kuondoka nyumbani.
“Tatizo
mwanamke anachelewa kurudi nyumbani, mumewe akimuuliza ndiyo mgogoro
unaanzia hapo,” kilisema chanzo hicho. Baada ya kunyetishiwa ‘ubuyu’
huo, Ijumaa Wikienda lilimsaka mume wa Jack, Dibibi ili kueleza ukweli
juu ya suala hilo.
‘Jack Pentzel’ na mumewe wakiwa kwenye picha ya pamoja na Rose Ndauka.
“Kutofautiana
ni jambo la kawaida na huwa tunagombana tu kawaida lakini siyo ugomvi
mkubwa kama watu wanavyosema. “Sijaondoka nyumbani, mbona nipo tu na mke
wangu, hao wanaosema hivyo wanataka kutukosanisha tu.”
Kumekuwa na uvumi wa kuvunjika kwa ndoa hiyo iliyofungwa mwanzoni mwa mwaka jana ambayo haijajaliwa kupata mtoto.
Post a Comment