Stori:  Mwandishi Wetu Aiseee!
 Ndoa ya binti aliyetambulika kwa jina moja la  Husna (16), imebuma 
baada ya bwanaharusi, Rahim (30), kuingia mitini muda mfupi kabla ndoa 
kufungwa.
Binti anayetambulika kwa jina moja la  Husna (16)(mwenye shela) , aliyetaka kuolewa na bwanaharusi, Rahim (30).
Tukio hilo la aina yake lilijiri maeneo ya
 Kitunda-Kati jijini Dar, 
wiki iliyopita ambapo chanzo makini kiliwajulisha Oparesheni Fichua 
Maovu (OFM) ya Global Publishers kwamba, kuna ndoa ya mtoto inafungwa 
kinyume cha sheria.
Baada ya kunyetishiwa ishu hiyo, OFM walitinga kwenye sherehe hiyo na
 kuanza kuwahoji baadhi ya ndugu ambao walikiri kwamba kweli ile ilikuwa
 ni ndoa ya mtoto aliyeacha shule akiwa kidato cha pili.
Akizungumza na OFM, Husna alisema aliamua kuolewa kwa sababu aliacha shule kutokana na kukosa ada.
Akizungumza na OFM, Husna alisema aliamua kuolewa kwa sababu aliacha shule kutokana na kukosa ada.
Alisema kwamba, darasani alikuwa haelewi chochote alichokuwa 
akifundishwa hivyo hakuwa na kazi yoyote.“Baba na mama yangu wameachana 
siku nyingi, sasa nilikuwa nalipiwa ada na mama huku kipato chake kikiwa
 ni kidogo.
“Niliamua kuachana na shule maana nilikuwa sielewi chochote kwa 
sababu niliugua mapepo, nimeamua mwenyewe kuolewa jamani maana sina kazi
 ya kufanya,” alisema Husna.Baada ya baadhi ya watu kuwashtukia OFM, 
walimpa taarifa bwanaharusi kwa simu na hakuonekana na ndoa hiyo 
ikaishia hewani kwani jamaa huyo hakufika kwa kuhofia hilo.
Mama akimfariji Husna
Baadhi ya ndugu wa bwanaharusi walikuja juu na kutaka warudishiwe 
mahari yao lakini mjomba wa mtoto huyo aliwasihi kwamba watakaa kama 
familia na watazungumza na wako tayari kurudisha mahari.
Baada ya ndoa hiyo kubuma, mtoto Husna aliangua kilio huku akisema kwamba anampenda huyo mchumba’ke huku mama yake naye akiangua kilio akidai anaumia kwani hajui atakapozitoa hizo fedha za mahari shilingi laki nne kwani kipato chake ni kidogo.

Post a Comment