Mwanamke ni mama mwenye nguvu unajua kwa nini kwa sababu mwanamke alitoka katika ubavu wa mwanaume baada ya Mungu kufanya yafuatayo kwa mwanaume..
A. Alimpa usingizi mwanaume
B. Alimfanyia upasuaji
C. Damu ilitoka kwa wingi kwa mwanaume
D. Nyama ilitolewa kwa mwanaume
E. Mfupa ulitolewa kwa mwanaume
F. Baada ya kufanyiwa hivyo mwanaume ndipo
mwanamke akaumbwa akatoka mwanaume akakiri na kusema huyo ni mfupa
katika mfupa wangu na nyama katika nyama yangu –hivyo ataitwa mwanamke
napenda ujue kuwa Mwanamke amebeba uponyaji wa mwanaume na mwanaume
amebeba vidonda kwa ajili ya mwanamke
Mwanamke ni mfupa mwanaume ni udongo hivyo mwanamke ni:
1. Ni nguvu ya mwanaume
2. Ni jasiri
3. Mchapakazi
4. Mwenye kujiamini
5. Tegemeo la familia
6. Mwalimu wa watoto na familia yake kiujumla
7. Mlinzi wa mwanaume – Bwana akisema ‘’nimefanya jambo jipya duniani mwamke atamlinda mwanaume
8. Chanzo cha baraka ya familia ( nitabariki Uzao wa tumbo lako)
9. Adui wa maadui wa familia (Uzao wa mwanamke utamponda kichwa nyoka na uzao wa nyoka (shetani ) utamponda kisigino (mwanzo)
10. Sauti ya familia (Bwana akamwambia Ibrahimu msikilize mkeo (mwanzo
11. Mponyaji wa familia yake na taifa
12. Mlezi wa huduma (wakamtumikia Yesu kwa mali zao(Luka8.3-4)
13. Mkombozi wa familia na taifa (kupitia mariamu mkombozi Yesu kristo alizaliwa (Luka i.29-35
14. Msaidizi wa Mungu tumfanyie msaidizi wa kufanana naye (mwanzo 2:18)
15. Mwombezi wa familia,huduma na taifa (Tuwapate wapi wa mama waombolezaji
16. Mficha siri wa Mungu (Rebbeca alificha ni nani atayekuwa mtawala
kati ya watoto wake wawili Esau na Yakobo.Baada ya kujua umuhimu wa
mwanamke tunatakiwa kuangalia kiundani sana tabia 30 za mwanamke bora
sio bora mwanamke tumeumia sana baada ya kuowa watu wasio sahihi katika
eneo lilosahihi mwanamke bora ni mwamuzi wa familia ndio mleta
mabadiliko katika familia mwanamke anayejua kwanini nipo hapa na
ninafanya nini?
Mimi nimefanya utafiki kutokana na vitabu na maisha yanayotuzunguka
nimeweza kugundua tabia 30 za Mwanamke anayeweza kunifaa mimi na wewe
rafiki yangu tuziangalie kwa makini sana na kwa utafiki wa ndani:-
1. Moyo wa Mwanaume humwamini:
Moyo wa M wanaume humwanini Mwanamke bora sio bora Mwanamke, Mwanamke
bora hujitahidi sana ili aweze kuaminika kwa mume wake maana Imani ni
kitu muhimu sana katika mahusiano, mahusiano yakipoteza Imani hapo
hakuna mahusiano, Mwanamke ana uwezo mkubwa sana wa kujiaminisha kwa
Mwanaume kuwa yeye ni mtu sahihi na chaguo sahihi kwa Mwanaume wake.
Moyo ndio unaothibitisha kuwa huyu ni mtu sahihi au sio sahihi
Moyo ndio unamkubari mtu
Moyo ndio sauti ya mwisho
Moyo ndio chanzo cha upendo
Moyo ndio jibu la maisha yako ya mapendo
Moyo ndio chemichemi ya mapenzi
Moyo ndio unaoamini na kinywa husema yaliyo maamuzi ya moyo.
Huyu
Mwanamke anatakiwa awe na jibu kwa Mwanaume- Upendo wa kweli
hautambuliki kwa muonekano wa mtu bali upendo huambulika toka moyoni:-
Hivyo Mwanamke bora ni Yule anayeweza kuushika moyo wa Mwanaume na
kujiaminisha kwake.
2. Huondoa umaskini
Mwanamke bora katika maisha yako ni Yule mwenye mawazo mazuri ya kuondoa
umaskini katika maisha yako- hana wazo baya, wengi wao wanatamani
kuolewa ili awe na sifa mtaani kuwa ameolewa lakini ni tegemezi, hana
wazo jipya la kubadilisha maisha yako. Hawa sio wanawake sahihi mawazo
yake yanamtegemea mwanaume, wazo lake ni kuzaa watoto hana wazo la
maendeleo, hajui maumivu ya maisha huwa wanarudisha nyuma ndoto zako
kutokutimia kwa wakati wake. Mwanamke bora ni Yule mwenye mawazo ya
maendeleo, mwenye hasira na umaskini mpenda mafanikio huyo ndiyo anafaa
kuolewa
3. Kamwe hamtendei Mume wake mabaya
Mwanamke bora yaani niniamaanisha aliye sahihi ni Yule mwenye moyo safi kwa mume wake,
1. Hawazi mabaya bali mema kwa mume wake,
2. Hawezi kumtendea mume wake mabaya,
3. Hawezi kumuumiza mume wake,
4. Hawezi kumtonesha vidonda mume wake,
5. Hawezi kuumsaliti mume wake,
6. Hawezi kumtendea yasiyo haki mume wake,
7. Hawezi kumchafua mume wake na kumdharirirsha katika jamiii iliyowazunguka,
8. Hawezikumtukana Mume wake,
9. Hawezi kushabikia maumivu na mateso ya Mume wake,
10. Hawezi kuwa radhi na maadui wa Mume wake,
11. Hawezi kuwa jeuri kwa Mume wake,
12. Hawezi kumtendea Mume wake mabaya.
13. Amejaa heshima kwa Mume wake,
14. Adabu,
15. Utu wema anatunza uthamani wa Mume wake
16. Amejaa utiifu na upole kwa Mume wake
17. Amejaa unyenyekevu na uaminifu kwa Mume wake,
18. Amejaa amani na furaha ya kweli kwa Mume wake-
19. Anayeshinda uovu kwa wema,
20. Mwenye upendo wa kweli kwa mume wake. Huyu ndiye Mwanamke unayeweza
kumuowa au kuishi naye na ndio sifa ya Mwanamke anayehitajika katika
maisha yako. Mwanamke huyu ataheshimika na kuthaminiwa na watu na
hatakosa upendo wa dhati kutoka kwa Mume wake.
4. Hufanya kazi kwa mikono yake kwa bidii
Mke bora sio bora Mke ni mchapa kazi ni mtafutaji kwa mikono yake
mwenyewe ni mjasiliamali hataki kuwa mzigo wa familia, kwa mikono yake
anajenga, kwa mikono yake anasomesha watoto wake, kwa mikono yake
anatunza familia yake kwa mikono yake anaheshimisha familia, mfanya kazi
kwa bidii asiyechoka usiku na mchana sio mvivu, kwa mikono yake
anafanya hategemei fedha za Mume wake- huyu anafaa kuwa Mke sahihi
katika maisha sio mlinda mlango ni mtafutaji anakufaa sana katika
maisha, napenda kukwambia mapenzi sio kuzaa, mapenzi kama pesa hakuna
hutaona udhamani ni wake pesa ni jawabu la kila kitu sasa Mwanamke
anajishughulisha anafaa sana katika maisha yetu ya leo- mapenzi ni
kusaidiana.
Mwanamke
sahihi hi Yule anayefanya kazi kwa mikono yake kwa bidii, Mwanamke
ningependa kukushauri kuwa mali za Mwanammme ni mali za watoto na mali
ya Mwanaume ni mali ya watu wengi, leo wanawake wengi wanateseka sana
baada ya waume zao kufa wamenyang’anywa mali zao na ndugu wa kiume
wanateseka sana kwa sababu walikuwa tegemezi kwa waume zao, Mwanamke wa
kweli ni Yule mtafutaji na kuwawekea watoto zake mazingira mazuri ya
maisha yao ya kesho.
5. Yeye ni kama meli ya biashara.
Mwanamke anafananishwa na meli ya biashara kwa sababu meli ya biashara
inachukua bidhaa mbali mbali ndani yake, Mwanamke amebeba majukumu mengi
sana katika maisha yake, mwanamke huyu ni:-
a) Mlinzi wa Mume wake.
b) Mzazi, mlezi mwenye watoto.
c) Mwangalizi mkuu wa familia yake na mazingira yake
d) Mwalimu Mkuu wa familia yake
e) Adui wa maadui wa familia yake.
f) Muombaji wa familia yake.
g) Kisima cha amani katika familia na ndugu wanaomzunguka.
h) Chanzo cha Baraka ya familia
i) Mficha siri ya familia- najua unajua kuwa Mwanamke ndio mficha siri
wa familia anajua yote yanayofanyika ndani. Mwanamke ana majukumu mengi
sana huku mtoto analia, baba naye anamwita huku watoto wanataka kusoma,
wakwe wanataka chakula na mavazi huyu anatakiwa kusaidiwa lakini
Mwanamke wa namna hii ndiye anayetakiwa katika maisha yako ndiyo maana
amefananishwa na meli ya biashara malalamiko amepewa yeye matusi yeye,
sifa njema yeye Mwanamke ni gari la familia. Nyumba yenye heshima
inamuhitaji Mwanamke sahihi.
6. Huleta chakula chake toka mbali,
Mwanamke bora hategemei kulishwa na Mwanaume anasifa yakutafuta chakula
chake toka mbali, hulisha familia yake kwa pesa yake, anahakikisha kuna
kila kitu kinachohitajika katika famila yake, tegemeo la Mume wake Mume
humwamini, nguzo ya familia yake, huyu ndiye Mwanamke anayetakiwa katika
maisha yetu, huyu anafaa ni chaguo lililo sahihi katika maisha yako.
7. Huamka kabla ya mapambazuko.
Mke bora huamka asubuhi na mapema kwa ajili ya kupanga mambo yake
ataamka na kufanya usafi ndani, mazingira yake kiujumla huandaa chakula
mapema hupangilia kazi kwa waliomo ndani mwake hufanya hivi na wewe
fanya hivi sio Mwanamke anayeamka saa tatu (3) asubuhi au saa nne (4)
asubuhi huyo ni mvivu hafai kuitwa Mwanamke bora bali ni bora Mwanamke
hafai hana faida katika kuchangia maendeleo maana hata maandiko
matakatifu yanasema “Siku njema huonekena alfajiri” mafanikio, Baraka,
amaendeleo, huanza asubuhi Mwanamke anyefaa utamwona anaamka asubuhi
sana na kupangilia mambo yake sawa, watu wa nyumbani watakula muda
sahihi, wataenda shule wakiwa wamejaa amani mwenye maneno mazuri juu ya
watoto wake na familia yake kwa ujumla. Huyu ndiyo Mwanamke anayetakiwa
katika maisha yako, sio wanaoamka muda wanaopenda, Mwanaume anaandaliwa
chai na mfanyakazi wa ndani, nguo za mume wako zinanyooshwa na
mfanyakazi, maji ya kuoga mume wako yanaandaliwa na mfanyakazi wa ndani
wewe sio Mwanamke sahihi na hufai kuitwa Mke bora wewe ni bora mke.
8. Hufikiri kununua shamba kisha hulinunua.
Mwenamke bora katika maisha hana mtazamo wa kununuliwa shamba, gari,
nyumba na chochote cha maendeleo yake na familia hufanya mwenyewe
akipenda kitu hununua hanunuliwi huyu ndiye Mwanamke wa Biblia mbunifu
wa maisha anayetazama mbali sana kwa fedha yake hufanya maendeleo
makubwa sana katika maisha yake, huyu ndiye Mwanamke bora anayefaa
katika maisha yetu ndiyo Mwanamke anayetafutiwa na watu wenye maendeleo.
Anaishi Kwa Jasho Lake, anategemea jasho Lake Hulima, hufanya kazi ili
awezekutimiza ndoto zake.
9. Huwa tayari kufanya kazi kwa nguvu
Mwanamke bora huwa tayari kufanyakazi kwa nguvu sana kwa ajili ya
familia yake, anajituma kwa bidii kwa kila shughuri anayoifanya, ni mama
mwangaikaji, mwenye kiu ya kutimiliza ndoto yake, mwenye kutambua
wajibu wake kitaifa na kifamilia, mwenye mtazamo wa mbali, mwenye kiu na
maendeleo, mwenye mzigo na familia yake, adui wa umaskini, ujinga na
maradhi, mwenye kujituma kabla ya kutumwa. Huyu ndiyo Mwanamke
anayetakiwa kuwa nayo katika maisha yake, huyu ndiye mama wa kibiblia
sio bora Mke ni Mke bora.
10. Mwenye kuthamini shughuri zake.
Mwanamke bora anathamini sana shughuri zake kuwa zinafaida anaikubali
kazi anayoifanya kuwa inafaa, hana tama na kazi za wengine ana heshimu
kazi yake sana, hatishwi na maendeleo ya wengine maana naye ni Mwanamke
anayejiamini sana kuwa hata yeye atafika, mwenye matumaini na Imani
kubwa kwa kile anachofanya. Huyu ndiye Mke anayefaa katika maisha
hutasikia malalamiko, hayupo katika mashindano, hana tamaa mbaya
ningependa kukushauri kuwa mwanamke anayekufaa sio Mwanamke akiona
mwenzake amevaa nguo Fulani naye anataka huyo hakufai ni muharibifu wa
maendeleo atakurudisha nyuma kimaendeleo, tafuta Mwanamke huyo hapo juu.
11. Hufanya kazi hata usiku kwa mwanga wa taa yake.
Mwanamke huyu mjasiliamali hata usiku hufanya mambo yake kwa ajili ya
maendeleo, hukanda unga wa maandazi, hushona nguo, vitambaa, hupanga
mambo yake kabla ya siku mpya, wenye kutambua wakati alionao, huyu ndiye
Mwanamke anaye kufaa katika maisha yako na ni Mwanamke wa kibiblia.
12. Asiye mchoyo.
Mwanamke bora sio mchoyo hufungua mikono yake kwa wahitaji, Mwanamke
mchoyo hakufai maana ananyima Baraka katika maisha yako, Mwanamke mchoyo
ni mchawi wa maendeleo, Mwanamke bora ni mtoaji, mwenye huruma na
wahitaji ni mlezi wa wengi, kioo cha fmailia mwenye roho ya msamaha, ni
mama wa wote walio wake na wasio wake, kwa aliyembariki na aliyemlaani,
hana ubaguzi, mwenye moyo wa mama wa kweli, mwangalizi wa wote. Huyu
ndiye mwanamke unaye muhitaji katika familia yako- usifanye makosa huyu
ndiyo Mwanamke wa kibiblia.
13. Hana hofu na maisha ya watoto wake.
Mwanamke bora huwa anahakikisha kuwa anawaandalia watoto wake maisha
mazuri, anawapeleka shule, msimamizi wa maendeleo yao, mtetezi wa haki
zao, anahakikisha watoto wake wanakuwa na nguo, elimu nzuri, afya nzuri,
kazi nzuri na anawaandalia maisha mazuri watoto wake hivyo anauhakika
na maisha yajayo ya watoto wake. Huyu ndiye Mwanamke anayetakiwa katika
maisha yetu.
14. Mwenye kujipenda
Mwanamke bora anajipenda sana, anajidhamini, ni mzuri sana, mwenye
kujikubali mwenyewe, adui wa uchafu, hawezi huwezi kumkuta mchafu hata
watoto wake wanaoga, anapiga mswaki, anapika mafuta yake mazuri, na
anaweka na marashi mwilini ili anukie vizuri sana, anatamanika, mavazi
yake mazuri sana, anamvuto aonekanapo wakati wowote nyumbani na nje ya
nyumba yake, Ua la familia, huyu ndiye Mwanamke anayetafutwa anamvuto wa
kuwanaye karibu, kutembea naye anayethanini usafi wa mwili wake kuanzia
chumbani kwake hadi nje huyu ndiye Mw anamke ninayekushauri uwe naye,
huyu ndiye Mwanamke wa kibiblia.
15. Mume wake hujulikana malangoni.
Mwanamke bora humtambulisha Mume wake malangoni, Mwanamke ni pazia ya nyumba,
1. Pazia husitiri mambo ya ndani,
2. Pazia hupendezesha nyumba,
3. Pazia mlinzi wa nyumba,
4. Pazia huthaminisha nyumba,
5. Pazia hutambulisha wakaao ndani ya nyumba,
6. Mwanamke ni pazia ya Mume,
7. Ndiye anayempendezesha Mume,
8. Mlinzi wa Mume
9. Ndiye anaye mthaminisha Mume,
10. Andiye anaye mtambulisha Mume,
11. Kioo cha Mume
12. Mwanamke ni pambola Mwanaume, kama nyumba ikikosa pazia ni rahisi
maadui kutambua vilivyomo ndani na kuvamia, ikikosa pazia hukaribisha
maadui, Mwanamke ni pazia la nyumba ndiyo anayemtambulisha Mwanaume hata
kama huyo Mwanaume ni mjinga Mwanmke anauwezo mkubwa wa kumuheshimisha
Mwanaume mbele za watu, Mwanamke ndio mlinzi wa Mwanaume. Mwanamke
anayejua wajibu wake hawezi kuibiwa Mume hata siku moja
“Sifa ya Mwanaume ni Mwanamke aliye naye”.
16. Mbunifu
Mwanamke bora nimbunifu wa maisha, hayuko nyuma huweza kufanya kitu na
hufanya, mbunifu wa biashara, mitindo ya mavazi, hubuni na kuwauzisha
wafanyabiashara, ni mtundu wa maendeleo, mwenye wazo jipy huyu ndiye
Mwanamke anayehitajika.
17. Mwenye nguvu na kuheshimika
Mwanamke bora ana nguvu za maendeleo mwenye mali inayopatikana katika
mikono yake mwenyewe na mwenye kuheshimika jamii inameshimu kwa
maendeleo yake, inamthamini, inamuogopa, ni kioo cha wa mama wengine
katika jamii inayomzinguka, mke bora anaheshimika na watu, ukiona
unadaraulika unatakiwa kubadilika maana Mke mwema ana nguvu katika jamii
na anaheshimika huyu huyu ndiye Mwanamke anayetakiwa katika maisha ya
leo.
18. Hucheka afikiriapo wakati ujao (Future)
Mwanamke bora hana hofu na wakati ujao maana amekweisha udhibiti wakati
ujao, Mwamnamke bora hutawala kesho hata kama hajaingia, hutawala jioni
wakati ni asubuhi hivyo hana hofu na mambo ya kesho, Mwanamke bora
anaucheka umaskini, magonjwa na ujinga huandaa mambo yake kwa wakati
aliopo na kwa wakati ujao, huyu ndio Mwanamke anayetakiwa asiyekuwa na
wasiwasi na kesho.
19. Hufungua kinywa Kunena kwa hekima.
Mwanamke bora amejaa hekima kinyuani SOPHIA - hekima ni kiongozi mzuri
sana katika maisha, ni mlinzi, hekima ni mtawala, hekima ni utajiri,
hekima ni heshima,
1. Mwanamke mwenye hekima hashindwi kuuitawala nyumba yake.
2. Mwanamke mwenye hekima hatishwi na watu na maneno yao.
3. Mwanamke mwenye hekima ni malkia wa nyumba yake,
4. Mwanamke mwenye hekima ni mkombozi wa familia yake.
5. Mwanamke mwenye hekima ni muamuzi wa haki katika familia yake,
6. Mwanamke mwenye hekima ni mdhibiti wa maovu katika famila yake.
7. Mwanamke mwenye hekima ni mponyaji wa famila,
8. Mwanamke mwenye hekima huondoa hasira kwa Mume wake.
9. Mwanamke mwenye hekima ni wa kujivunia,
10. Mwanamke mwenye hekima ni mponyaji wa ndoa yake/ huyu ndiyeMwanamke
anaye tafutwa katika maisha yetu rafiki wa wote huyu ndiye Mwanamke
anayehitajika katika maisha.
20. Huwashauri wengi kwa wema.
Mwanamke bora ni mshauri mzuri kwa wengine, mwenye kushauri mema wala
sio mabaya kwa watu waliomzunguka yaani ni mponyaji wa familia za watu
wengi hata taifa, ushauri wake hauna madhara kwa watu, kimbilio la
wengi, sio mwenye mwenye kuharibu ndoa za watu, mchonganishi,
mshirikina, muongo hapana, Mwanamke anatakiwa kutoa ushauri mzuri kwa
wengi huyu ndiye Mwanamke tunayemuhitaji wengi.
21. Huchunguza yote yanayofanyika nyumbani mwake.
Mwanamke bora anakuwa makini sana na kila kitu kinachoendelea au
kutendeka katika nyumba yake anakuwa mwangalifu sana mna mambo ya
nyumbani kwake kwa sababu yeye ndiye msimamizi mkuu wa nyumba yke,
anatakiwa awe na muda wa kutosha na nyumba yake, hapendi ujinga nyumbani
mwake, mahali pa kuonya anaonya, mahali pa kufundisha nafundisha, yeye
ndiye mratibu mkuu wa yote yanayotendeka nyumbani, yeye ndiye kiongozi
wa nyumba yake, mtendaji mkuu wa nyumba yake ndiye mjenzi wa familia
bora hivyo Mwanamke kama huyu anyejua mjukumu yake ndiye anayetakiwa
katika maisha yetu, sio kila Mwanamke umuonaye anafaa.
22. Kamwe hakai bure hata kidogo
Mke bora hakai bure lazima atakuwa na kitu cha kufanya, huwezi kumkuta
kwenye vikao vya umbea, anazunguka zunguka kwenye nyumba za watu, maana
ana mambo ya kufanya hakai bure hata kidogo ni mchapa kazi, anajituma,
mbunifu wa mambo, anautaratibu wa maisha yake. Mwanamke ambaye yupo yupo
tu huyo hatufai,ni chanzo cha matatizo, umbea, muongo, tafuta Mwanamke
anayechapa kazi yuko (busy) na shughuri za kifamilia, kiofisi mwenye
maendeleo huyo ndiye Mwanamke anayefaa katika maisha.
23. Watoto wake huamka na kumshukuru.
Mke bora watoto wake wanafuraha naye, wanamshukuru sana mama yao, maana
amewajengea maisha mazuri amewafundisha mambo mazuri, amewalea vizuri,
watamuheshimu sana mama yao na kumpenda, watamlinda na kumtunza mama ,
mama wa kweli husifiwa na watoto wake, watoto wanajisikia amani
wanapokuwa naye, mwenye maadili mema mbele ya watoto wake,. Mfano wa
kuigwa kwa mambo mazuri anayowatendea watoto wake hivyo shukurani
hazitaweza kundoka midomoni mwa watoto wake huyo ndiye Mwanamke
anayetakiwa.
24.Mume huimba sifa zake
Mke bora Mume wake humsifia kwa sifa njema Mume hutangaza uzuri wa Mke
wake, hutangaza mtendo mazuri ya Mke wake, hujivunia na anajisikia
bahati kuwa na mke kama huyo, mwenye tabia njema, mtiifu, mpole katika
maisha yake mwenye kujiheshimu, anyempenda mume wake na watoto zake,
msema kweli, mlinzi mwaminifu, Mwanamke mwenye maendeleo huyu ndiye
Mwanamke anayetakiwa katika maisha yetu aliyekubarika katika moyo wa
Mume wake mpenzi.
24. Mwenye kumcha Mungu
Mke bora ni Yule mcha mungu anayempenda Mungu mtu wa Ibada mwenye hofu
ya Mungu anayeichukia dhambi, mpenda maombi na Neno la Mungu huyu ndiye
Mke sahihi katika maisha, mwenye mzigo wa maombi kwa ajili ya Mume wake
na watoto wake na wote waliomzunguka huyo ndiye chemichemi ya mabadiliko
ya familia, mleta ukombozi wa fmailia huyu ndiye Mwanamke anayefaa
katika maisha yetu ya leo.
25. Mwenye kupenda elimu.
Mke bora ni Yule anyependa Elimu. Elimu imegawanyika katika sehemu
mbili. Kuna Elimu inayopatikani mashuleni na Elimu inaopatikana katika
mazingira unayoishi, wazazi na jamii iliyokuzunguka Mke bora anapenda
kujifunza mazuri kwa wengine, mafanikio yao, sio mjuaji, yupo tayari
kurekebishwa na kubadilika, anayekubari kushauriwa huyo ndiye Mwanamke
anayefaa maana ni msikivu na mpenda mabadiliko yenye faida
26. Huandaa chakula kwa familia yake.
Mke bora ni mpishi mzuri wa chakula katika familia yake hategemei
wafanyakazi yeye ni Mwalimu wa wengine mume humsifia Mkwa kwa mapishi
yake mazuri nay a usafi wa hali ya juu sana . mpendwa najua unajua kuwa
kuna baadhi ya wake za watu hawajui kupika, sio mbunifu wa mapishi
mchafu katika maandalizi yake huwa ni wake wasio bora, wanavunja nyumba
zao, tafuta Mke ambaye hana chakula cha kukariri bali bali ni mbunifu wa
mapishi ni msafi anayejipenda mwalimu wa mapishi huyo ndiye Mwanamke
anayetakiwa katika maisha yetu ya leo.
27. Mwenye sifa njema.
Mke mwema anasifa njema katika jamii iliyomzunguka hana tabia za uzinzi
na uasherati, hana tabia ya ulevi na matusi, hana tabia ya umbea na
uchonganishaji, hana tabia ya kiburi na jeuri Mke mwema ni rafiki wa
watu wengi amejaa shukrani na hana mawazo mabaya Mke bora hutambulika na
matendo yake katikajamii inayomzunguka.
28. Mwenye kudhamini na kutunza upendo.
Mke bora anajua maana ya upendo na gharama zake, anajua maumivu na
vidonda vya mapenzi, anajua nguvu ya upendondani ya mtu, anatambua hisia
kali ya upendo, Mwanamke wa namna hiyo hataweza kukusaliti,
atakuheshimu na kukupenda kweli kutoka moyoni mwake hatagawa upendo
wakko kwa wengine, atalinda penzi lake kwa ajili yako, anaheshimu mwili
wake huyu ndiye Mwanamke anayetafutwa anayejua kwanini umempenda yeye na
umewaacha wengine mwenye tabia njema. Huyu ndiye Mama wa familia bora
sio bora familia.
29. Mwenye wivu wa maendeleo
Mke bora ana wivu wa maendeleo hana wivu wa kijinga unaoweza kusababisha
amani katika ndoa kuondoka .Mwanamke ni mponyaji wa ndoa yake ni kweli
Mwanamke anatakiwa awe na wivu kwa Mume wake lakini vilevile lazima awe
na Imani na Mume wake, kuna wivu unaoweza kuharibu amani ya nyumba
lakini kuna wivu unaoweza kujenga nyumba. Inategemea Mama ana wivu wa
namna gani sio wote walio karibu na Mume wako, wako katika mahusiano na
Mume wako, Mwanamke bora hufanya utafiti wa jambo na kuwa na uhakika
naolo na huliwasilisha kwa hekima sana. Wivu ni mzuri ukitumiwa vizuri
na pendo la kweli lina wivu lakini uwe wa maendeleo katika maisha yenu
Post a Comment