Hakuna mtu asiyejua maana ya watoto wa kishua basi kama yupo basi maana halisi ya neno hili ni wale watoto waliozaliwa kwenye familia zinazojiweza au unaweza kuita familia Bora. Mara nyingi wasanii wengi huwa wanatokea maisha duni na kupigana na maisha hadi kufikia walipo sasa. Kipindi Diamond akiacha shule kwa kukosa pesa ya kumsomesha nana elimu yake kuishia A’level , Hawa wengine walikua wapo shule wakisoma na kuishi vizuri. BongoSwaggz inawaorodhesha baadhi ya watoto wakishua ambao kwasasa ni celebrities.
Vanessa Mdee au
unaweza kumuita Vee au Vee Money alizaliwa mjini Arusha mwaka 1988.
Vanessa mdee alikuzwa na baba yake Sammy Mdee (kwasasa ni marehemu
)ambaye alikua ni mtu mzito kwenye nchi hii na mama yake sophia. Akiwa
na umri mdogo Vanessa aliweza kusafiri nchi mbalimbali duniani. Vanessa
Mdee alikulia miji ya New York , Paris , Nairobi na Arusha.
2:NISHER
NisherNisher
ni mtoto wa Mtumishi wa Mungu Mh Nabii GeorDavie anayeongoza huduma ya
Ngurumo ya Upako yenye makao yake jijini Arusha. Nisher amekulia katika
maisha mazuri na hadi ni wakishua bado. Baba yake aliweza kumsaidia
Nisher kufungua studio yenye thamani kama ya milioni 15 ili mtoto wake
aendeleze kipaji alichonacho.
3:JOKATE KIDOTI
Jokate MwengeloHuyu
unaweza kumuita mtoto wa Oysterbay kwani ndio alipokulia huku baba yake
akifanya kazi serikalini. Kumbuka Jokate alizaliwa washington DC nchini
Marekani ambapo wazazi wake walikua wakifanya kazi huko. Alipomaliza
high school katika shule ya Loyola ndipo alipogombania Miss Tanzania
mwaka 2006 na kushika nafasi ya 2.
4:PRODUCER LUCCI
LucciJina
lake halisi anaitwa Luciano Tsere au unaweza kumuita Lucci ambaye ni
producer maarufu nchini. lucci amezaliwa tarehe 30 September mwaka 1985
Lusaka Zambia, akiwa ni mzaliwa wa nne, wa mwisho kuzaliwa na akiwa
mtoto wa kiume pekee kwenye familia yao. Lucci naye kama jokate amekulia
Obey kwenye familia bora ambapo kwasasa mzee wake ni balozi wa
Tanzania.
5:WEMA MSEPETU
5:WEMA MSEPETU
Wema SepetuWema
Sepetu ni msichana anayetoka kwenye Familia ya kibalozi akiwa ni mtoto
wa mwisho katika familia ya wasichana wanne wa Balozi Isaack Sepetu
Ibrahimu (marehemu).Wema sepetu alizaliwa mnamo mwaka 1988 katika
hospitali ya ST. Andrew’s jijini Dar es Salaam na ni mtoto wa mwisho
kuzaliwa huku akisoma elimu yake ya primary na sekondari katika shule ya
ACADEMIC INTERNATIONAL iliyopo jijini Dar es Salaam kabla ya kwenda
Nchini Malaysia kusomea mambo ya biashara za kimataifa katka chuo cha
Limkokwing University.
Post a Comment