Idris ambaye alinyakua kitita hicho nchini Afrika Kusini wikiendi 
iliyopita, aliwasili jana nchini na kupokelewa na Wabongo wengi ambao 
walimpongeza kutokana na ushindi huo alioupata baada ya kuwagaragaza 
washiriki saba wa nchi tofauti za Afrika.
Siku alipotangazwa ushindi, kesho yake 
(Jumatatu) Lulu ndiye aliyekuwa mtu wa kwanza kutupia picha ya zamani 
katika mtandao wa Instagram akiwa na Idris na kuacha gumzo kwa wafuasi 
wa mtandao huo juu ya ukaribu huo kiasi cha kupiga picha ya pamoja.
Elizabeth Michael ‘Lulu’ akipozi.
Picha hiyo ilizua gumzo huku kila shabiki akisema lake, kuna ambao 
walimpongeza kwa kuwa na urafiki na nyota huyo mpya lakini wengine 
wakaponda.“Jamani tuache ushamba yeye amempongeza tu kama alivyokuwa 
akifanya tangu zamani, kwani kuna ubaya?” alihoji mdau mmoja.
Mbali na Lulu, baadaye wasanii wengine walifuata mkumbo huo wa kuweka
 picha wakiwa na Idris ambazo wengi walikuwa na lengo la kumpongeza 
mshindi huyo ingawa Wabongo wengi walidai kuwa wanajipendekeza.Katika 
mazungumzo yake na mwanahabari wetu, mbali na mipango mingine, Idris 
amepanga kuwekeza sehemu ya fedha zake katika soko la filamu Bongo.  
 
Post a Comment