Msichana Kulwa Joseph (21) mwenye ulemavu wa ngozi (albino) mkazi wa 
kijiji cha usonga kata ya sirambo wilayani kaliua mkoani tabora, 
amenesurika kuuawa na majambazi watatu, ambapo awali walimteka Balozi wa
 nyumbakumi na kumpiga ili awapeleke kwa mlemavu huyo naye kwa kubaini 
nia mbaya akawapeleka nyumba nyingine.
Akizungumza katika kituo cha kulelea yatima na wanaoishi 
katika mazingira hatarishi cha huruma kilichoko chini ya kanisa 
katholiki, Binti huyo lkulwa Joseph amesema kuwa, watu ambao 
hawakujulikana walivamia nyumbani kwa jirani na kuanza kuwapiga mjomba 
wake anayeishi nyumba ya jirani.
Mkuu wa wilaya ya kaliua Bw Saveli Maketa ambaye alimnusuru kwa 
kumhamisha porini walipokuwa anaishi amesema kuwa hali ya maisha ya 
walemavu wa ngozi wilayani humo inaonyesha kuwa hatarishi ambapo 
amewataka wananchi kuwa na mshikamano ili kuwanusuru na hali hiyo. 
Mratibu wa chama cha wenye uremavu mkoani Tabora Bw, Focus 
Magwesera amemtaja balozi aliyejeruhiwa na majambazi hayo kwa jina la 
makoye meli ambapo katika kutaka kumnusuru mlemavu huyo, aliwapeleka 
majambazi hao kwa nyumba ya jirani, huku mwenyekiti wa walemavu wilaya 
ya Sirambo akitishiwa kuuawa.
 

Post a Comment