Msanii wa Sanaa ya 
Maigizo Nchini, Elizabeth Michael almaarufu kama Lulu akiongea na 
waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa Alipokuwa akiitambulisha 
filamu yake Mpya iitwayo MAPENZI YA MUNGU ambayo amewashirikisha Flora 
Mtegoha au Mama Kanumba na Msanii wa Muziki wa Kizazi Kipya Linah Sanga.
 Msanii Wa Maigizo 
Nchini, Elizabeth Michael almaarufu kama Lulu akiitambulisha filamu yake
 Mpya iitwayo MAPENZI YA MUNGU leo mbele ya wanahabari (hawapo 
pichani).,Kulia ni Mmoja kati wa wasanii walioshiriki katika filamu hiyo
 ajulikanae kama Flora Mtegoha almaarufu kama Mama Kanumba
Meneja Masoko wa 
Kampuni ya Proin Promotions Ltd, Evance Stephen akiongea na wanahabari 
leo katika Ofisi za Proin Promotions Ltd zilizopo Mikocheni mtaa wa 
Ursino wakati wa Utambulisho wa Filamu mpya ya Lulu Iitwayo MAPENZI YA 
MUNGU.
Msanii Elizabeth 
Michael aka Lulu leo ametambulisha Filamu yake Mpya ambayo imeingia 
sokoni leo iitwayo MAPENZI YA MUNGU, huku akiwa amemshirikisha Msanii wa
 Bongo Fleva Linah Sanga na Mama Kanumba.
Wakati akiilezea 
filamu hiyo leo mbele ya wanahabari Lulu amesema Kuwa Ni Filamu 
inayofundisha na Kutoa somo kwa mtu yoyote yule ambae yupo hapa duniani 
kwa kuendelea kuonyesha kuwa MUNGU YUPO. Akiongezea kuwa..."Sisi kama 
binadamu tumekuwa tukifanya mambo mengi sana hapa Duniani na kupelekea 
kumsahau Mungu na pengine kuendelea kufikiria kuwa yote tuyafanyayo ni 
kwa uwezo wetu kumbe Sio uwezo wetu na Ni Mapenzi ya Mungu tu ndio 
yanayofanya sisi kufikia hapa tulipo leo"
Filamu ya MAPENZI YA 
MUNGU imekuwa gumzo kabla ya kutoka kutokana na watanzania wengi kuwa na
 shauku ya Kutaka kumuona Lulu tena mara baada ya Kuonekana  katika 
Filamu Zake Mbili zilizotangulia za FOOLISH AGE na FAMILY CURSE. Sasa 
Lulu kuonekana tena katika kiwango cha Juu katika Filamu hii Mpya ambayo
 imeingia Sokoni Leo.
Filamu ya MAPENZI YA MUNGU ni filamu inayosambazwa na Kampuni ya Proin Promotions Ltd.
 
Post a Comment