Wiki hii kupitia safu hii tunaye Maimartha Jesse ‘Mai’ ambaye ni mtangazaji na mjasiriamali. Mwandishi wetu Hamida Hassan alimbana kwa maswali 10 mengi yakiwa yanahusu mambo ya chumbani zaidi, ungana naye…
TQ: Ni chakula gani kizuri ambacho ukimpikia mumeo anasikia raha?
Mai: Mume wangu ni mpenzi sana wa wali samaki au ugali samaki, sambamba na vikorombwezo vingine.
TQ: Ukiwa sebuleni na mumeo mkiangalia vipindi mbalimbali vya televisheni ni mavazi gani unavaa na mapozi gani mnakaa?
Mai: Huwa tunakaa kwa heshima tu kwa sababu nina familia na wakati wote inakuwa karibu yetu.
TQ: Vipi uwapo chumbani na mumeo unapendelea kumtega kwa mavazi gani au nakshi zipi?
Mai: Kiukweli
kule hakuna kuvaa nguo, ni cheni ya kiunoni, vikuku mguuni kwani
tunakuwa wawili tu. Si unajua tena pale ndiyo eneo la kujidai na laazizi
wangu?
TQ: Kwa mapenzi hayo mnayooneshana, siku ikitokea umemfumania mumeo na mwanamke mzuri kuliko wewe, utachukua uamuzi gani?
Mai: Siwezi
kumuacha mume wangu kwa sababu jiji hili lina wanawake wabaya ambao
wanajipeleka wao kwa wanaume. Nitakachokifanya ni kumvalisha mume wangu
nguo kisha namrudisha nyumbani. Nikifika namuandalia juisi bariiidi.
Baada ya hapo nitaenda kumalizana na mwizi wangu.
TQ: Utamfanya nini huyo mwizi wako?
Mai: Ukweli ajiandae kwa viwembe kwani nitahakikisha nimemchakaza sura yake, akitoka hapo akiona mume wa mtu atamuogopa kama ukoma.
TQ: Inasemekana una hausigeli mkali sana, vipi siku mumeo uzalendo ukimshinda na ukawakuta kwenye kitanda mnacholala?
Mai: Hilo
haliwezi kutokea. Unajua nimeshamsoma mume wangu na kugundua hawezi
kujivunjia heshima yake kwa kutembea na mfanyakazi wetu, ila siku
ikitokea ndiyo nitajua cha kufanya.
TQ: Kuna haka kaskendo ka’ mastaa wengi kujihusisha na usagaji? Wewe umeshawahi kushiriki kwa namna yoyote?
Mai: Huo ni uchafu, anayefanya hivyo maisha yamemshinda, hutasikia hata siku moja mimi nimefanya ujinga huo.
TQ: Inadaiwa wewe kwa kuchepuka ni noma na una kidumu chako (mwanaume wa pembeni), taarifa hizi zina ukweli wowote?
Mai: Heshima
niliyonayo kwa kuitwa mke wa mtu siwezi kuitia doa, najiheshimu sana
kuliko watu wanavyofikiria. Huwezi kuamini mimi nawashangaa sana
wanaochepuka.
TQ: Kabla ya ndoa umewahi kutoka na wanaume wangapi?
Mai: Kiukweli idadi ipo ila sipendi kuitaja kwa kuwa nahisi nitamkwaza mume wangu .
TQ: Kuna madai kuwa shepu uliyonayo Mchina anahusika sana, hebu funguka.
Mai: Hayo ni mambo yangu binafsi sipendi kuyaongelea bwana, kila mmoja ana maisha yake aliyoyachagua.
Post a Comment