Ikiwa
ni wiki 2 tu zimepita baada ya bibi aliyedhaniwa kuwa mchawi (80)
kukutwa nje ya nyumba ya mtu akiwa uchi hajitambui katika mtaa wa
Mageuzi kata ya Ndembeza mjini Shinyanga,matukio yanayohusishwa na imani
za kishirikina yameendelea kuacha watu midomo wazi ambapo leo asubuhi
binti anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 23- 25 aliyedaiwa kuwa mchawi
amekutwa hajitambui akiwa amevaa nguo nyeusi,kashikilia chungu kidogo
kwenye mlango wa nyumba ya mtu katika mtaa wa Bushushu kata ya Lubaga
katika manispaa ya Shinyanga huku akidai kuwa amefika mahali hapo kwa
kutumia chungu
Wakazi
wa Shinyanga wakiwa eneo la tukio nje ya nyumba aliponasa binti huyo
anayedhaniwa kuwa mchawi kutokana na nguo alizovaa na dawa nyeusi
alizopaka kwenye mwili wake.Binti
huyo kwamba alifika mahali hapo na wenzake kufanya sherehe baada ya
kufanikisha uchawi wao wa kuharibu ndoa ya Massawe aliyegoma kuoa ndugu
yao na badala yake akaoa mwanamke mwingine.
Tukio
hili limetokea leo asubuhi katika mtaa wa Bushushu nyumbani kwa
Robinson Massawe ambapo binti huyo alikutwa amelala mbele ya mlango wa
nyumba hiyo akiwa hajitambui na baada ya kusemeshwa ndipo akasimulia
yaliyomkuta kwamba alifika mahali hapo na wenzake zaidi ya 10 kutoka
kanda ya ziwa kufanya sherehe baada ya kufanikisha uchawi wao wa
kuharibu ndoa ya Massawe ili ndugu yao aolewe na baba wa familia
hiyo.Kwa mujibu wa ndugu wa baba mwenye nyumba wameiambia Malunde1 blog
kuwa kweli ndoa hiyo ilivunjika tangu tarehe 17.9.2014
Pichani binti aliyejitambulisha kwa jina la Coletha akiwa
amevaa kishirikina huku mwili wake ukiwa umepakwa dawa nyeusi akidai
kuwa alikuwa anaongoza wenzake zaidi ya 10 Geita,Mwanza na Shinyanga
kuwanga katika nyumba hiyo.Baada ya kukutwa hapo mlangoni wakazi wa eneo
hilo walifika eneo la tukio kisha mwenyekiti wa mtaa huo Ruben Masanja
akimwomba mwenye nyumba amruhusu binti aingie ndani kwa usalama wake
Post a Comment