0

Hakikisha mnakwenda sawa kila hatua. Furaha yenu itadumu kama tu ninyi wote mtaamua kwa pamoja. Mapenzi siyo sinema kusema wahusika ni wengine, kazi yako ni kuzama matukio yanavyoendelea. Unatakiwa uhusike na mchezo wenyewe kwa asilimia 100.
Kuna tatizo ambalo lipo kwa baadhi ya wanawake, hushindwa kutambua kuwa faragha inahusisha watu wawili. Kwa maana hiyo, mmoja peke yake hawezi. Hivyo basi, kama ambavyo hutakiwi kufanya namna yako unayojua mwenyewe, naye pia haruhusiwi. Kushirikishana ni muhimu.
Tengenezeni muunganiko kuanzia mwanzo na hakikisheni mnaenda kwa spidi inayowiana mpaka mwisho wa safari yenu. Wapo ambao huenda waavyojua wao, wanapokaribia kileleni hawawaambii wenzi wao, matokeo yake mtu anakuwa anatoa macho, hajitikisi.
Hasemi kitu na kwa sababu alishafika mwisho, kile kitendo huanza kukiona kero kwake. Ikiendelea zaidi hulalamika anaumia, zaidi ya hapo humshurutisha mwenzi wake amalize. Kuna nyakati humlazimisha wakatishe na kweli mechi inafikia ukingoni wakati mwanaume hajatikisa nyavu.

Hiyo ni tabia mbaya, ni ubinafsi. Kama kweli unampenda mwenzi wako hutakubali kushiriki naye bila mawasiliano ya hatua kwa hatua. Kumbuka kwamba mnachokifanya siyo kitendo cha ubakaji, umeridhia kwa moyo wako mkunjufu. Unataka raha, sasa utazipataje ikiwa kila mmoja anafanya anachokijua?
Nilishasema kuwa kitanda kina kanuni zake. Kuna makosa mengi hufanywa na wanawake, vilevile yapo ambayo wanaume huyafanya. Si sawa kuyaacha yaendelee kuwepo kwa sababu faragha ni hatua muhimu katika ukamilishaji wa kitu kinachoitwa penzi.
Uhusiano wa kimapenzi una wigo mpana. Kuna mambo mengi ambayo yakifanywa hukufanya uwe na afya. Hata hivyo, suala la faragha halipaswi kusahaulika, kwa maana ni chachandu madhubuti.
Tendo la faragha lina nguvu sana katika kuuweka hai uhusiano. Wapo watu ambao picha zilikuwa haziendi katika maisha ya kawaida lakini kila wakikutana kitandani, kila mmoja alimvulia kofia mwenzake.
Hii ina maana kuwa inawezekana mwenzi wako akawa dhaifu katika maeneo mengine lakini ‘maujuzi’ yake faragha, yakakufanya uwe mtulivu kwake. 
Vivyo hivyo, nawe hakikisha unampatia mwezi wako katika eneo fulani ili hata akikufanyia visa, basi uwe na ukurasa wako ambao akiufikia ni lazima akuvulie kofia. Faragha ni uwanja huru ambao hudhani ni mgumu lakini ni rahisi sana.
Haihitaji msuli mkubwa wala nguvu kama za Simba. Usidanganyike kwenda kutumia madawa ya kuongeza nguvu wala kwenda kwa waganga eti ndiyo wakuboreshee mvuto wako. Tuliza kichwa, soma kitendo chenyewe halafu hakikisha hufanyi makosa.
Ka kifupi ni kwamba mambo mengi hayahitaji taaluma, ni suala la kuushirikisha ubongo ili uamue kinachotakiwa. Mathalan; kuzungumza na mwenzi wako kumuuliza nini umfanyie ili afurahie tendo au kumwelewesha cha kufanya aweze kukupatia, haihitaji maarifa mengi au uwezo wa juu kiakili.
Kujifanya unajua sana husababisha wengi kuchemka. Achana na tabia ya kuhisi wewe umekamilika na kujidanganya kwamba unafahamu kila kinachotakiwa katika uwanja mahsusi wa faragha. Inakugharimu kiasi gani kuzungumza naye ili akujuze mahali hisia zake zilipolalia?
Yupo mwanamke ambaye tangu anazaliwa mpaka anakua, amekariri kwamba ukiwa faragha dawa ni kuzungusha ‘bakuli’ mwanzo mwisho. Matokeo yake, anakutana na mwenzi wake, badala ya kusoma mahitaji yake, yeye akili, nguvu na ujuzi wake wote anauelekeza katika nyonga tu. Mauno mtindo mmoja.
Hajui kwamba pengine mwenzi wake hapendi purukushani za kupanda na kushuka. Inapotokea wewe ni mtaalamu wa kucheza juu ya msumari (wana wa unyago mnaelewa), dakika 90 hushushi mzigo chini, ukidhani unamfurahisha, kumbe unageuka kero kwa mwezio. (Hii niliwahi kueleza katika matoleo yaliyopita).
Tukutane wiki ijayo kuchambua mambo mengine sita yaliyobaki kwa kasi, nguvu na ari zaidi.

Post a Comment

 
Top