0

JAMAA anayedaiwa kwamba ni mpambe mkubwa wa mmoja wa wagombea urais mwakani ambaye ni fundi wa kufunga madishi, mkazi wa Magomeni-Makanya jijini Dar es Salaam, almaarufu Mgosingwa, amejikuta akivishwa shanga baada ya kunaswa na mke wa mtu chumbani kwake. 
Mgosingwa akivishwa shanga baada ya kufumaniwa na mke wa mtu. FUMANIZI
Tukio hilo la aina yake la kufungia mwaka 2014 lilijiri kwenye fumanizi la jamaa huyo lililochukua nafasi nyumbani kwake maeneo ya Magomeni-Makanya, Dar, Jumanne iliyopita ambapo alifumwa na mke wa jamaa aliyejitambulisha kwa jina moja la Faki aitwaye Mwanahamisi akidaiwa kumrubuni kwa nguo za Sikukuu ya Krismasi. 
Kwa mujibu wa mwenye mke, baada ya Mgosingwa ambaye mkewe alikuwa safarini, kunaswa laivu alitaka kuchoropoka kupitia dirishani lakini jamaa alimkamata miguu na kumrudisha ndani. 
OFM
Kama kawa, makamanda wa Oparesheni Fichua Maovu (OFM) ya Global Publisher wanaotumia bodaboda ziendazo kasi, walitonywa na kufanikiwa kufika eneo la tukio ndani ya dakika sifuri.
...Akiwasihi wamuachie baada ya kufumaniwa. OFM walipofika walikuta mtiti umeshika kasi ambapo kabla ya kufikia hatua ya kudhuriana, polisi waliokuwa doria mtaani waliitwa na wasamaria wema na kwenda kuokoa jahazi. 
AVISHWA SHANGA
Polisi walipofika walimkuta mwenye mke akiwa na shanga mkononi akimvalisha Mgosingwa ambaye tayari hakuwa na ujanja.Hata hivyo, polisi hao walifanya kazi ya ziada kumdhibiti mwenye mke ambaye alikuwa akipambana nao akitaka aachiwe apambane na mgoni baada ya kumvisha shanga. 
MAYOWE
“Niacheni jamani lazima na mimi leo nim….(tusi), haiwekani kabisa mtu atake kumdhalilisha mke wangu.
“Mke wangu nitajua cha kumfanya tukifika nyumbani, yaani ukweli nampenda sana mke wangu,” alisikika mwenye mke akipiga mayowe.
Dk. Wilbrod Slaa,
 WAAMRISHWA WAVAE NGUO
Tukio hilo lilisababisha mjumbe wa nyumba kumi wa eneo hilo aliyejitambulisha kwa jina la Mama Vicky na Afisa Mtendaji wa Mtaa wa Makanya (hakutaja jina) wafike eneo hilo na kuwaamrisha waliofumaniwa wavae nguo kwanza. 
SERIKALI YA MTAA
Baada ya kuvaa, wahusika wote walipelekwa kwenye ofisi ya mtendaji wa mtaa huo ili wazungumze na ikiwezekana wayamalize kwani wahusika hao walikuwa ‘hawajaduu’ bado.
January Makamba. 
MSAMAHA
Baada ya kufika ofisi ya mtendaji, Mgosingwa alimpigia magoti mwenye mke na kumuomba msamaha huku akikiri kuwa alikuwa akitaka kula tunda la mkewe lakini alikuwa bado hajathubutu kufanya hivyo hata siku moja. 
“Chondechonde kaka, mimi ni mwanaume mwenzako na wote, mimi, wewe na mkeo tunatoka pamoja pale Makorora (Tanga) na familia zetu zinajuana fika.“Naomba unisamehe ndugu yangu niko tayari kukulipa fidia ya kunishika ugoni,” aliomba Mgosingwa. 
Mgosingwa aliendelea kuomba radhi ambapo mjumbe wa nyumba kumi na afisa mtendaji walimshauri mwenye mke kupunguza jazba kisha akubali kuzungumza na mgoni wake, wasifike mbali na kuyamaliza ili kuepusha usumbufu. 
Benard Membe. 
FAINI MIL. 1.5
Baada ya kushauriwa kwa muda mrefu, mwenye mke aliiheshimu mamlaka hiyo ya serikali na kukubali kulipwa faini shilingi milioni moja na nusu za Kitanzania ili kumsamehe mgoni na kumpa onyo kali endapo wataendeleza kamchezo hako.Baada ya hapo, Mgosingwa aliendelea kuwapigia simu ndugu zake wamtumie fedha kwenye simu ili amalize tatizo hilo. 
NI MPAMBE WA MGOMBEA GANI?
Kwa mujibu wa majirani wa Mgosingwa ni mpambe wa mmoja wa wanasiasa maarufu anayedaiwa kuwa kwenye ‘resi’ za kugombea urais mwakani, kufumaniwa kwake kumetajwa pia kama ni njia mojawapo ya kumchafua mgombea huyo.Mgosingwa alipoulizwa kama ni mpambe wa mgombea gani hakuwa tayari kutaja.
Waziri mkuu Mizengo Pinda. WANAOTAJWA URAIS 2015
Baadhi ya vigogo wanaotajwa kutaka kugombea urais kwenye Uchaguzi Mkuu 2015 ambao wana wapambe kila kona Bongo ni pamoja na Mizengo Pinda, Benard Membe, January Makamba, Frederick Sumaye, Dk. Khamis Kigwangala, Dk. Wilbrod Slaa, Wiliam Ngeleja, Steven Wasira, Dk. Mohamed Shein, Dk. Emmanuel Nchimbi, Dk. Asha-Rose Migiro na Edward Lowassa.

GPL

Post a Comment

 
Top