0

CHRISTIAN BELLA AKIWA NA KAKA YAKE TAYARI KWA SHOW YAKE NCHINI HOLLAND
Pichani ni mwimbaji nyota wa muziki wa dansi Christian Bella akiwa na kaka yake katikati ya jiji la Amsterdam nchini Holland tayari kwa onyesho lake jijini humo.
Katika onyesho hilo litakalofanyika Jumamosi hii, Christian Bella atashirikiana na kaka yake Zoe Bella (pichani kushoto) ambaye ni mwimbaji wa kiwango cha kimataifa.
Zoe Bella aliwahi kuimba kwenye bendi ya Koffi Olomide, Quartier Latin.

Bella ameiambia Saluti5 kuwa anajaribu kuutangaza muziki wa dansi kutoka Tanzania katika nchi kadhaa za Ulaya ili kufungua milango kwa wasanii wengine wa dansi, hasa kutokana na ukweli kuwa soko la muziki huo ni dogo sana.

Post a Comment

 
Top