0

Mwanamke mmoja Swaumu Aboubakari mwenye miaka24 mkazi wa Keko Jijini Dar es salaam ambaye ni mjamzito amenusurika kufa baada kupigwa na vitu vyenye ncha kali na mzazi mwenzake kutokana na ugomvi wa kifamilia.

Akizungumza kwa shida katika wodi alikolazwa Hospitali ya Mwananyamala alisema ameishi na mzazi mwenzake kwa takribani miaka mitano huku ndoa yao ikitawaliwa na migogoro kila wakati.

Alisema baada ya Mateso kuongezeka alichukua uamuzi wa kurudi nyumbani kwa wazazi wake akiwa na mtoto wake mwenye umri wa mwaka mmoja huku akiwa na ujauzito mwingine.

Alisema juzi usiku alitoka Keko kwenda Tandale kwa mzazi mwenzake kwa ajili ya kuomba fedha za matumizi lakini akiwa ndani ya nyumba yake mwanaume huyo alitoka sebuleni na kumchukua kwa nguvu mtoto na kwenda kumlaza chumbani na aliporudi alianzisha ugomvi akishirikiana na ndugu zake akimuhumu mwanamke huyo kuwa mimba si yake.

“Mume wangu bila hata huruma akishirikiana na ndugu zake walinipiga kwa kutumia waya,rungu,fimbo na chuma,sehemu mbalimbali za mwili na nimejaa vidonga kama mnavyoona”alisema Mwanamke huyo.

Post a Comment

 
Top