
Mkali huyo wa filamu Afrika Magharibi alithibitisha hilo, kupitia
mtandao wa kijamii wa Twitter huku akimsifia mlimbwende huyo kwamba ni
mwigizaji mzuri.
“Kitu changu kingine kikubwa, nimefurahia muunganiko baina ya Ghana
na Tanzania, ni siku ya kwanza lakini nimefurahishwa na namna
tulivyoweza kuifanya kazi hii kwani unajua nini unakitaka. Nimefarijika
kufanya kazi na wewe, katika filamu hii itakayojulikana kwa jina la ‘Day
After Death’, mhusika mkuu ni Wema Sepetu na mimi,” aliandika katika
mtandao wa huo alfajiri ya jana.Kusoma zaidi bofya
Van Vicker aliweka wazi kuwa filamu hiyo aliyoiongoza, ilimpa wakati
mgumu lakini anafurahia changamoto alizopewa na mlimbwende huyo.
“Katika filamu hii watazamaji pia watawaona mabinti zangu wawili ambao wameigiza ndani yake.”
Meneja wa Wema, Martin alisema kuna kazi kadhaa zinazofanywa chini ya Kampuni ya Endless Fame na kampuni ya Van Vicker kwa sasa.
“Van Vicker kupitia kampuni yake ya Sky + Orange Productions ambayo
yeye ni mkurugenzi mkuu na Wema kupitia Endless Fame akiwa mkurugenzi
mkuu pia, wameungana kufanya mradi na tayari wameshafika nchini Ghana
kwa ajili ya kukamilisha kazi hizo,” alisema Kadinda na kuongeza: “Huu
ni mradi mkubwa ambao wanauandaa utakaojumuisha kampuni hizi mbili, kwa
hiyo mashabiki wake wategemee makubwa inaweza kuwa filamu au vinginevyo
wasubiri matokeo, Wema ameongozana na Petitman mmoja kati ya wafanyakazi
wa kampuni.”
Wema aliandika katika ukurasa wake wa Instagram: “Tupo katika matayarisho.”
Chanzo:Mwananchi
Post a Comment