 JAMAA
 anayedaiwa kwamba ni mpambe mkubwa wa mmoja wa wagombea urais mwakani 
ambaye ni fundi wa kufunga madishi, mkazi wa Magomeni-Makanya jijini Dar
 es Salaam, almaarufu Mgosingwa, amejikuta akivishwa shanga baada ya 
kunaswa na mke wa mtu chumbani kwake.
JAMAA
 anayedaiwa kwamba ni mpambe mkubwa wa mmoja wa wagombea urais mwakani 
ambaye ni fundi wa kufunga madishi, mkazi wa Magomeni-Makanya jijini Dar
 es Salaam, almaarufu Mgosingwa, amejikuta akivishwa shanga baada ya 
kunaswa na mke wa mtu chumbani kwake. 
Mgosingwa akivishwa shanga baada ya kufumaniwa na mke wa mtu. FUMANIZI
Tukio hilo la aina yake la kufungia mwaka 2014 lilijiri kwenye 
fumanizi la jamaa huyo lililochukua nafasi nyumbani kwake maeneo ya 
Magomeni-Makanya, Dar, Jumanne iliyopita ambapo alifumwa na mke wa jamaa
 aliyejitambulisha kwa jina moja la Faki aitwaye Mwanahamisi akidaiwa 
kumrubuni kwa nguo za Sikukuu ya Krismasi. 
Kwa mujibu wa mwenye mke, baada ya Mgosingwa ambaye mkewe alikuwa 
safarini, kunaswa laivu alitaka kuchoropoka kupitia dirishani lakini 
jamaa alimkamata miguu na kumrudisha ndani. 
OFM
Kama kawa, makamanda wa Oparesheni Fichua Maovu (OFM) ya Global 
Publisher wanaotumia bodaboda ziendazo kasi, walitonywa na kufanikiwa 
kufika eneo la tukio ndani ya dakika sifuri.
AVISHWA SHANGA
Polisi walipofika walimkuta mwenye mke akiwa na shanga mkononi 
akimvalisha Mgosingwa ambaye tayari hakuwa na ujanja.Hata hivyo, polisi 
hao walifanya kazi ya ziada kumdhibiti mwenye mke ambaye alikuwa 
akipambana nao akitaka aachiwe apambane na mgoni baada ya kumvisha 
shanga. 
MAYOWE
“Niacheni jamani lazima na mimi leo nim….(tusi), haiwekani kabisa mtu atake kumdhalilisha mke wangu.
“Mke wangu nitajua cha kumfanya tukifika nyumbani, yaani ukweli nampenda sana mke wangu,” alisikika mwenye mke akipiga mayowe.
 WAAMRISHWA WAVAE NGUO
Tukio hilo lilisababisha mjumbe wa nyumba kumi wa eneo hilo 
aliyejitambulisha kwa jina la Mama Vicky na Afisa Mtendaji wa Mtaa wa 
Makanya (hakutaja jina) wafike eneo hilo na kuwaamrisha waliofumaniwa 
wavae nguo kwanza. 
SERIKALI YA MTAA
Baada ya kuvaa, wahusika wote walipelekwa kwenye ofisi ya mtendaji wa
 mtaa huo ili wazungumze na ikiwezekana wayamalize kwani wahusika hao 
walikuwa ‘hawajaduu’ bado.
MSAMAHA
Baada ya kufika ofisi ya mtendaji, Mgosingwa alimpigia magoti mwenye 
mke na kumuomba msamaha huku akikiri kuwa alikuwa akitaka kula tunda la 
mkewe lakini alikuwa bado hajathubutu kufanya hivyo hata siku moja. 
“Chondechonde kaka, mimi ni mwanaume mwenzako na wote, mimi, wewe na 
mkeo tunatoka pamoja pale Makorora (Tanga) na familia zetu zinajuana 
fika.“Naomba unisamehe ndugu yangu niko tayari kukulipa fidia ya 
kunishika ugoni,” aliomba Mgosingwa. 
Mgosingwa aliendelea kuomba radhi ambapo mjumbe wa nyumba kumi na 
afisa mtendaji walimshauri mwenye mke kupunguza jazba kisha akubali 
kuzungumza na mgoni wake, wasifike mbali na kuyamaliza ili kuepusha 
usumbufu. 
FAINI MIL. 1.5
Baada ya kushauriwa kwa muda mrefu, mwenye mke aliiheshimu mamlaka 
hiyo ya serikali na kukubali kulipwa faini shilingi milioni moja na nusu
 za Kitanzania ili kumsamehe mgoni na kumpa onyo kali endapo 
wataendeleza kamchezo hako.Baada ya hapo, Mgosingwa aliendelea kuwapigia
 simu ndugu zake wamtumie fedha kwenye simu ili amalize tatizo hilo. 
NI MPAMBE WA MGOMBEA GANI?
Kwa mujibu wa majirani wa Mgosingwa ni mpambe wa mmoja wa wanasiasa 
maarufu anayedaiwa kuwa kwenye ‘resi’ za kugombea urais mwakani, 
kufumaniwa kwake kumetajwa pia kama ni njia mojawapo ya kumchafua 
mgombea huyo.Mgosingwa alipoulizwa kama ni mpambe wa mgombea gani hakuwa
 tayari kutaja.
Baadhi ya vigogo wanaotajwa kutaka kugombea urais kwenye Uchaguzi 
Mkuu 2015 ambao wana wapambe kila kona Bongo ni pamoja na Mizengo Pinda,
 Benard Membe, January Makamba, Frederick Sumaye, Dk. Khamis Kigwangala,
 Dk. Wilbrod Slaa, Wiliam Ngeleja, Steven Wasira, Dk. Mohamed Shein, Dk.
 Emmanuel Nchimbi, Dk. Asha-Rose Migiro na Edward Lowassa.
GPL
 
Post a Comment