Aliyekuwa
Miss Tanzania 2014, Sitti Abbas Mtemvu katika pozi na mshindi wa pili,
Lillian Kamazima (kulia) pamoja na mshindi wa tatu, Jihhan Dimachk.
Mshindi
wa Miss Tanzania 2014 Sitti Mtemvu, kwa hiari yake mwenyewe bila
kulazimishwa na mtu ameamua kulivua rasmi taji hilo la urembo.

Akiongea na
EATV mratibu wa shindano hilo Hashimu Lundenga amesema kuwa Sitti
Mtemvu ameamua kwa maamuzi yake binafsi na sio wao kama kamati ya Miss
Tanzania.
"Sababu
kubwa ya Sitti kulivua taji hilo ni baada ya kuchoshwwa na maneno mengi
yaliyozushwa juu yake, maana pia aliitwa na RITA kwaajili ya uchunguzi
zaidi hivyo ameona mambo yanazidi kuzushwa mengi hivyo ameamua kulivua
taji hilo". Amesema Hashimu Lundenga
Baada ya Sitti Mtemvu kulivua taji hilo atavalishwa aliyekuwa mshindi wa pili Lilian Kamazima
Post a Comment